Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Katavi
(Mpanda Hospitali)

TAARIFA SAHIHI YA HUDUMA ZETU HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA KATAVI

Posted on: September 21st, 2025


Mnamo tarehe 20/9/2025 kuna Mdau aliuliza swali kwa viongozi,Kwamba kwa nini watu wengi Mpanda Katavi wanalalamika huduma za afya katika Hospitali kuu ya Rufaa ya Katavi?

Aidha kuna Wadau kadhaa walitoa mchango wao wakisema,

Unatozwa hela kisha unaambiwa hakuna dawa, unafika saa 2 kisha unahudumiwa saa 10 tena chini ya kiwango, Kausha Damu na Madaktari pia kuambiwa ni Wapigaji.

Hospitali inapenda kutoa ufafanuzi juu ya Upotoshaji huu kuhusu Huduma zetu:

  • Kuanzia mwaka 2024 mpaka sasa hospitali ya Rufaa ya Mkoa imeongeza huduma za madaktri bingwa ambazo hapo awali hazikuwepo kama vile
  • Daktari Bingwa Bobezi upasuaji wa mifupa
  • Daktari Bingwa upasuaji wa Koo,Pua na Masikio
  • Bingwa Upasuaji wa Mfumo wa Mkojo
  • Bingwa upasuaji wa Macho
  • Bingwa Afya ya Akili
  • Huduma mpya ya Uchujaji Damu (Dialysis) ambapo mpaka sasa tumeshafanya zaidi ya mizunguuko 250 ya kusafisha Damu, aidha Wagonjwa wote waliokuwa wamehama Mpanda sasa wamerejean Katavi kuendeleza huduma hii.
  • Aidha Wagonjwa wetu wote wanaohitaji huduma hizo za kibingwa huwa wanaonwa eneo maalumu, na kwa siku maalum,na Kama amelazwa kuna Jopo la madaktari linapita pia.
  • Kusema kwamba Huduma zinatolewa chini  ya kiwango na huku Daktari Bingwa amekuona ni kuupotosha Umma.
  • Kuhusu Dawa kuwa hazipatikani taarifa hii sio ya kweli,Kwa mwaka wa fedha 2024/2025 Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ina upatikanaji wa Dawa zaidi ya 99% na kila siku kuna ufuatiliaji wa ukosefu wa dawa yoyote. Na mwaka huu ulioisha Hospitali ya Rufaaa ya Mkoa imepata Cheti cha Pongezi (Recognition Award) kutoka Bohari kuu ya Dawa (MSD) kati ya hospitali 28 za rufaa za Mikoa kwa manunuzi na ulipaji kwa kutumia vyanzo vya ndani.
  • Kuhusu Gharama za Hospitali kuwa juu pia ni Upotoshaji mkubwa, kwani Bei zote za Huduma za Afya ni Bei elekezi za Serikali kwa ngazi ya Rufaa kuanzia Dawa mpaka Vipimo na Huduma nyinginezo. Aidha hakuna Mgonjwa anayekosa huduma Hospitali ya Rufaa ya MKoa kwa kushindwa kulipia huduma, kwa sababu kuna utaratibu maalum wa kupatiwa musamaha wa muda/kudumu kupitia Ustawi wa jamii na kwa siku tu ni kati ya milioni moja mpaka tatu za fedha zinasamehewa kutoa huduma.
  • Kuhusu Muda wa Kuona Wagonjwa, Hospitali imejiwekea utaratibu kwamba ndani ya NUSU SAA baada ya kusajiliwa, Wateja wetu wanatakiwa wawe wameonana na Daktari na kusubiri vipimo. Aidha mud awa kukaa hospitali kupata huduma inategemea aina ya Ugonjwa, Idadi ya Vipimo na aina ya vipimo, hivyo muda hutofautiana sana kwa muktadha huo.
  • Huduma kwa Wateja (Cuatomer care Centers), Hospitali ya Rufaa ya Mkoa kwa kutambua umuhimu wa kutoa Huduma Bora na za Kiwango ilianzisha Dawati/Vibanda vya huduma kwa wateja ambapo vipo maeneo mawili ndani ya hospitali ambapo waweza kupata maelezo ya huduma, msaada,usaidizi au kama hujaridhishwa na huduma zetu. Vibanda hivyo vimeelezea haki yako kama mteja na wajibu wa mtoa huduma (Client service Charter),sambamba na hilo kuna namba za simu za Viongozi wa Taasisi na akiwemo Afisa ustawi wa jamii ili wateja wetu waweze kutoa maoni juu ya huduma zetu kupitia namba hizo.
  • Kutoa taarifa ya huduma kupitia na Kupokea maswali/maoni kupitia Mpanda FM. Uongozi mara kadhaa umefika katoa masomo/kupokea maoni na kujibu baadhi ya maswali kutoka kwa wateja wetu,tumefanya na tunaendelea kufanya hivyo ili kuujuza Umma wa wanakatavi juu ya huduma zetu,na kuwa huru kuchangia maoni pale ambapo wanaona kuna maeneo ya kuboresha.
  • Tunatoa wito kwa Jamii ya wanakatavi,Wanahabari, Wadau wetu wote Mfike Hospitali ya Rufaa ya Mkoa kupata taarifa sahihi ya huduma zetu zilivyoimarika hasa katika kipindi ambacho Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imewekeza vya kutosha sekta ya Afya takribani maeneo Miundombinu, Dawa na Vifaa Tiba, Pamoja na Rasilimali watu.
  • Pamoja na Maelezo hayo juu tunapenda kuambatisha na baadhi ya picha zinazoonyesha uboreshaji wa Huduma zetu, na ikiwa utakuwa na Maoni tafadhali usisite kutupigia kwa namba zilizohapo chini.
  •              
  • IMETOLEWA NA KITENGO CHA  MAHUSIANO KWA UMMMA.